Wanawake washauriwa kukuza kipato cha familia
31 January 2023, 12:07 pm
“Wanawake wa Mkoani Mtwara wameshauriwa kupambana katika kutafuta na kuongeza kipato cha familia na kuachana na tabia ya kuwaacha wanaume pekee katika kutekeleza majukumu ya Nyumbani.“
Na Mohamed Massanga
Akizungumza na Jamii fm Radio Mwenyekiti wa kikundi cha ‘’LIYAKAYA WOMENI GROUP’’ kinachopataikana Mtawanya juu mtaa wa Zahanati Bi Rabia Halidi Zuberi amewataka wanawake wenzake kujishughulisha na kazi mbalimbali katika kuiongezea familia kipato.
“Wanawake tusibweteke kwa kukaa kusubiri wanaume kutuletea mahitaji ya nyumbani badala yake wapambane na kusaidia majukukumu ya wanaume majumbani.
“Wanawake tusibweteke kwa kukaa kusubiri wanaume kutuletea mahitaji ya nyumbani badala yake wapambane na kusaidia majukukumu ya wanaume majumbani.”
Nao wanachama wa kikundi hicho wamesema kuwa kuna faida kubwa ya kuwa mwanakikundi kwani wamefanikiwa kuondoa changamoto za kifamilia kama vile mahitaji ya watoto ya shule na mengineyo huku wakiomba pia viongozi wa kata kuwa na utaratibu wa kutembelea vikundi vilivopo kwenye maeneo yao utawala ili kujua changamoto wanazo pitia.