Mwenge wa uhuru kupitia miradi 62 yenye thamani ya Bilioni 30.09 Mtwara
30 May 2024, 13:32 pm
Na Musa Mtepa
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala leo tarehe 30/5/2024 amepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea mkoani Lindi katika Viwanja vya shule ya Msingi Mpapura halmashauri ya Mtwara Vijijini.
Akiongea wakati wa mapokezi ya Mwenge huo mkuu wa mkoa Sawala amesema kuwa Mwenge wa uhuru katika mkoa wa Mtwara utakimbizwa katika umbali wa kilomita 906.6 kwa kupitia miradi 62 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 30.09
Aidha RC Sawala amesema kuwa mbio za mwenge wa uhuru utakimbizwa katika Wilaya sita,Halmashauri tisa na ukitarajiwa kukabidhiwa mkoani Ruvuma baada ya siku tisa kuanzia tarehe 30/5/2024.
Pamoja na hayo RC Sawala ametumia nafasi hiyo kuelezea maandalizi na shughuli mbalimbali zilizofanywa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kushirikiana na ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa kuwa ni Pamoja na uhakiki wa maeneo ya utawala na kubaini idadi ya wapiga kura.
Mh Kanali Patrick Sawala amekabidhi Mwenge wa uhuru kwa mkuu wa wilaya ya Mtwara ambayo ambayo ndio wilaya ya kwanza kukimbiza Mwenge huo katika mkoa wa Mtwara ambapo utakimbizwa katika halmashauri ya Mtwara mjini, Mtwara vijijini na halmashauri ya mji Nanyamba
Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 unachagizwa na kauli mbiu ya “Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu”