Zaidi ya wakimbiaji 100 washiriki Mikindani Marathon
29 June 2024, 13:13 pm
Mikindani Marathoni Marathoni ni sherehe zinazoambatana na maadhimisho ya siku ya mikindani(Mikindani day) ambayo dhima ni kutangaza utalii wa mji mikindani ,utamaduni wa makabila ya mikindani(Mtwara) pamoja na historia mbalimbali za mji huo.
Na Musa Mtepa
Katika kusheherekea kilele cha siku ya Mikindani (Mikindani day) Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala mapema leo Juni 29,2024 ameshiriki Mikindani Marathoni katika mji Mkongwe wa Mikindani ambapo zaidi ya wakimbiaji 100 wameshiriki katika marathoni hiyo.
Akizungumza wakati wa mbio hizo RC Sawala amesema ni siku ya kihistoria kwa mkoa wa Mtwara katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo mji Mkongwe wa Mikindani na mkoa wa Mtwara kwa ujumla kupitia marathoni na michezo mbalimbali iliyofanyika katika kilele hicho.
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala
Kwa upande wake katibu mkuu wa kamati ya Olympiki Tanzania Filbert Bayi amefarijika kuona uwepo wa Mikindani Marathon huku akitaka hamasa kuongezeka kupitia kwa wadau na wanamtwara kushiriki katika mbio hizo kwani zinaweza kuzalisha wakimbiaji wazuri wanaoweza kuwakilisha Mtwara na nchi kimataifa.
Sauti ya Filbert Bayi katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania
Naye Mshindi wa Mbio za kilomita 21 Haji Kajao (CHAMPIONI) amesema anatamani kuona Mikindani Marathoni yakiendelea kwa kila Mwaka kwani imekuwa ikileta hamasa kwa vijana na inaweza kuwa sehemu ya kuonesha vipaji vyao.
Guakisa Mwasyeba na Shabani Majidi washindi wa pili na watatu kwa mbio za kilomita 21 ambapo wameshukuru kushiriki katika Marathoni hiyo huku wakitoa ushauri kwa washiriki kutambua afya zao kabla ya kushiriki.
Sauti ya Guakisa Mwasyeba na Shabani Majidi Washindi wa pili na wa tatu katika Mikindani Marathon kwa umbali wa kilomita 21
Mikindani Marathoni zimehusisha katika umbali wa kilomita 21,km 10,km 5 na km 2.5 zenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika mji mkongwe wa Mikindani Pamoja na utamaduni wa watu wa pwani na mkoa wa Mtwara kwa ujumla.