MAKALA – Ladha ya chakula kilichopikwa kwa nishati ya Gesi
29 April 2023, 14:52 pm
Na Musa Mtepa
Kutokana na kukuwa kwa Technolojia Binadamu ameweza kubadilika na kuendana na mazingira husika yanayoendana na mabadailiko hayo ambayo sio tu kwa wakazi wa mijini bali hata katika maeneo ya Vijijini.
Zamani ukienda vijijini na kukutana na Mzee kikongwe ukimuuliza ni nishati gani mlikuwa mnaitumia katika kupikia atakuambia alikuwa anatumia nishati ya kuni kitu ambacho ni tofauti na watu wasasa ambapo kutokana na kukua kwa technolojia hali imekuwa tofauti watu wanatumia nishati ya gesi kwenye mapishi na hata nishati ya umeme.
Nikukaribishe kwenye kipindi hiki cha Mazingira na Gesi ambapo hii leo tunaangazia matumizi ya nishati ya gesi za mitungi majumbani jinsi gani inavyotumika na vyakula gani vimekuwa vikipikwa kupitia ishati hiyo.
Mwaandaaji na Msimuliaji wa KIpindi hiki ni mimi Musa Mtepa