Jamii FM

Watu wenye ulemavu wahimizwa kushiriki  uchaguzi serikali za mitaa

28 September 2024, 10:20 am

Bw Abdala Saidi Adam akiwa katika Studio za jamii fm redio akitoa wito kwa watu wenye ulemavu kushiriki katika michakato ya uchaguzi (Picha na Musa Mtepa)

Abdala Saidi Adam ni mlemavu wa macho aliyefanikiwa kupata elimu ya sekondari ya kidato cha nne na kufaulu lakini alishindwa kuendelea na masomo kutokana na hali ngumu ya Maisha ya wazazi wake hivyo akalazimika kurudi nyumbani na kuendelea na Maisha mengine

Na Musa Mtepa

Watu wenye ulemavu wametakiwa kushiriki kikamilifu katika michakato mbalimbali ya uchaguzi ili waweze kuchagua viongozi watakaowatetea katika changamoto wanazokabiliana nazo katika maisha yao ya kila siku.

Wito huo umetolewa Septemba 25, 2024, na Abdala Saidi Adamu, aliyekuwa mwenyekiti wa watu wenye ulemavu katika kata ya Madimba, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Dira ya Asubuhi kinachorushwa na Jamii FM Radio.

Bw. Adamu amesema kuwa, kutokana na changamoto wanazopitia, ni muhimu kwao kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili waweze kupata viongozi watakaowakilisha maslahi yao.

Sauti ya Saidi Adamu aliyewahi kuwa  mwenyekiti wa watu wenye ulemavu kata ya Madimba

Aidha, kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, Bw. Adamu ameonyesha nia ya kugombea nafasi ya mwenyekiti wa kijiji ili iweze kuwa rahisi kutatua kero zinazowakabili watu wenye ulemavu.

Sauti ya 2 Bw Saidi Adamu mlemavu wa macho aliyewahi kuwa menyekiti wa watu wenye ulemavu kata ya Madimba.

Pia, Bw. Adamu ametumia fursa hii kuwaomba Watanzania kumpatia msaada wa kifedha kupitia nambari ya simu( 0653 454 106), ili kumwezesha kugharamia mahitaji ya shule ya mtoto wake, ikiwa ni pamoja na unifomu, viatu, madaftari, na chakula.