Pembejeo za ruzuku zawafikia wakulima Mtwara
28 June 2023, 14:50 pm
Mchakato wa ugawaji wa pembejeo ya ruzuku kwa wakulima wa zao la korosho umeanza kuwafikia wakulima katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumzia mchakato huo Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndugu Francies Alfred amesema kuwa kwa miaka miwili iliyopita ugawaji wa pembejeo ulikuwa unasimamiwa na vyama vikuu vya ushirika kugawa pembejeo hizo hali iliyopelekea changamoto ya upotevu hivyo kulazimika kubadilisha mfumo huo.
Sambamba na hilo Bw Francis amesema kuwa kwa wale wote ambao walishindwa kujisajili katika awamu ya kwanza ya usajili watasajiliwa awamu ya pili na matarajio ya upatikanaji wa pembejeo ni kwa awamu ya pili pia.
Aidha mkurugenzi mkuu wa bodi ya korosho ametolea ufafanuzi juu ya utolewaji wa pembejeo ya ruzuku inayotolewa na serikali huku akiwataka wakulima kutotegemea pembejeo ya ruzuku pekee katika kuhudumia mashamba yao.