Jamii FM

Umuhimu wa mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu

27 November 2025, 18:01 pm

Tuma Dandi ambaye ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa Televison ya Taifa TBC1. Picha na Amua Rushita

Akiwa ni mtu mwenye ulemavu wa viungo, amejitolea kuitumia taaluma yake kuibua na kusimulia hadithi za jamii, hususan za watu wasiojiweza na watu wenye ulemavu.

Na Msafiri Kipila

Katika jamii inayozingatia usawa wa haki na fursa, ni muhimu kila mwananchi kupata huduma za kijamii kwa usawa bila vikwazo, Uwepo wa mazingira rafiki husaidia watu wote, hususan watu wenye ulemavu, kupata huduma kwa urahisi na kwa kujitegemea bila kulazimika kuomba msaada wa mara kwa mara.

Katika kipindi hiki, tupo na Tuma Dandi, mwandishi wa habari na mtangazaji maarufu wa televisheni na vyombo vya habari nchini Tanzania. Tuma Dandi ni mtangazaji wa kipindi cha Wape Nafasi kinachorushwa na TBC1 (Shirika la Utangazaji Tanzania). Akiwa ni mtu mwenye ulemavu wa viungo, amejitolea kuitumia taaluma yake kuibua na kusimulia hadithi za jamii, hususan za watu wasiojiweza na watu wenye ulemavu, kwa lengo la kuhamasisha jamii, wadau na mamlaka husika kutoa msaada na kufungua fursa mbalimbali.

Ungana nasi kusikiliza kipindi hiki kwa kubonyeza hapa muhimu ili kujifunza, kuelewa na kuchangia katika ujenzi wa jamii jumuishi yenye mazingira rafiki kwa wote.