Jamii FM

CHADEMA yahimiza wananchi kupima uwezo wa wagombea badala ya vyama vya kisiasa

25 November 2024, 23:57 pm

Dadi Mpisu mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Mtwara Vijijini akinadi sera za chama kwa wananchi wa kijiji cha Ngorongoro(Picha na Musa Mtepa)

Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa kampeni zinatarjia kuhitimisha kesho tarehe 26.11.2024 saa 12:00 jioni   ikiwa tayari kwa ajili ya uchaguzi November 27, 2024

Na Musa Mtepa

Wananchi wa Kijiji cha Ngorongoro, Kata ya Nanguruwe, Halmashauri ya Mtwara Vijijini, wametakiwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuzingatia uwezo wa kiongozi atakayekabiliana na changamoto za wananchi, badala ya kuangalia jina la chama cha kisiasa.

Dadi Mpisu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Mtwara Vijijini, ameeleza kuwa kiongozi bora ni yule atakayejenga Kijiji cha Ngorongoro kwa kushirikiana na wananchi bila kujali tofauti za kisiasa.

Sauti ya 1 Dadi Mpisu mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Mtwara vijijini.

Pia amewahamasisha wananchi kufanya mabadiliko katika vijiji vyao na kutoa nafasi kwa vyama vingine ili kuondoa changamoto zinazowakabili, hususan katika sekta ya kilimo cha korosho na huduma za afya, ambazo mara nyingi zimekuwa changamoto kubwa kwa jamii.

Sauti ya  Dadi Mpisu mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Mtwara vijijini.

Aidha, Saidi Mohamedi Mnwele, Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Nanguruwe, amesema kuwa wao kama viongozi wamejipanga vyema kuhakikisha wanashinda na kuchukua nafasi za uongozi, kuanzia kwenye nafasi ya uenyekiti wa vijiji na vitongoji.

Sauti ya Saidi Mohamed Mnwele Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Nanguruwe.

Kwa upande mwingine, Mgombea wa Uenyekiti katika Kijiji cha Ngorongoro, Bi Fatuma Fakihi, hakufika kwenye mkutano wa kampeni kutokana na kusumbuliwa na homa, kama alivyosema Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Nanguruwe.

Kampeni hizi ni sehemu ya mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo wananchi wanahamasishwa kuchagua viongozi watakaowasaidia kutatua changamoto za kijamii.