Mafundi umeme wa Mtwara na Lindi wapewa elimu
25 November 2021, 13:17 pm
Nawaomba wananchi kuwatumia mafundi Umeme walio na leseni, wao ndio wenye ufanisi wa kazi ambao tunawatambua na itasaidia endapo mtu utapata changamoto una uwezo wa kuja EWURA kufungua malalamiko tofauti na yule ambae amefanyiwa kazi na fundi ambae hana leseni.
Meneja EWURA kanda ya mashariki Mhandisi Nyirabu Musira
Na Grace Hamisi;
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) imewapa mafunzo ya siku tatu mafundi umeme walio na leseni kwa mikoa ya lindi na mtwara, na yalifanyika kwenye ukumbi wa veta mkoani mtwara huku mgeni rasmi akiwa
Mkuu wa wilaya ya mtwara Dustan Kyobya kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo mkuu wa wilaya amewahasa mafundi kutengeneza mazingira mazuri kwa viongozi ili iwe rahisi kitambua uwepo wao kwa jamii na waweze kupewa kazi kwa wenye leseni
Hata hivyo kwa upande wa kiongozi wa mafundi umeme bi engeltraud edmund mbemba amesema mafunzo hayo yatawaongezea uelewa zaidi lakini pia ameiomba serikali kuliangalia swala la vishoka kwani ni changamoto kwa upande wao kukosa kazi za kufanya.
Aidha kwa upande wa meneja EWURA kanda ya mashariki Mhandisi Nyirabu Musira amewaomba wananchi kuwatumia mafundi umeme walio na leseni kwa wao ndio wenye ufanisi wa kazi ambao unatambulika na itasaidia endapo mtu atapata changamoto ana uwezo wa kwenda EWURA kufungua malalamiko na kesi yako tofauti na yule ambae amefanyiwa kazi na fundi ambae hana leseni.