Jamii FM

Halmashauri zapewa mwezi mmoja kutenga eneo la kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi

25 June 2024, 20:13 pm

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala akizungumza na viongozi mbalimbali waliohudhuria utambulisha wa programu ya Imarisha Uchumi na Samia(IMASA) uliofanyika kwenye ukumbi wa BOT mjini Mtwara(Picha na Musa Mtepa)

Programu ya Imarisha Uchumi na Samia ni Programu inakuja kuboresha shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wananchi ambayo itakuwa na mfumo wa usajili kwa kila mmoja au kikundi kwa kutumia namba ya NIDA,akaunti ya Benki na kutoa taarifa za mtaji alionao,biashara anayofanya .

Na Musa Mtepa

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amezitaka halmashauri zote za mkoa  wa Mtwara kutenga maeneo kwa ajili ya kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi(one Stop centre) ili viweze kusaidia Wananchi katika shughuli zao za kiuchumi.

Agizo hilo amelitoa leo Juni 25,2025 kwenye  utambulisho wa Programu ya Imarisha Uchumi na Samia (IMASA) chini ya uratibu wa Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki kuu (BOT) mjini Mtwara ambapo Kanali Sawala amesema kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu mtendaji wa Baraza hilo inaonesha kutokuwepo kwa kituo cha uwezeshaji hivyo ni wajibu wa kila halmashauri ndani ya mwenzi mmoja kuanzia sasa hadi July 30 ,2024 kila halmashauri kutenga eneo kwa ajili ya kituo cha uwezeshaji Wananchi kiuchumi.

Sauti ya 1 Kanali Patrick Sawala mkuu wa Mtwara

Aidha Kanali Patrick Sawala amesema hatarajii kuona watu wakianzisha vikundi ambavyo havipo (fake) na matarajio ni kuona vikundi halisi vinasajiliwa na sio vinginevyo huku akiwataka wakuu wa wilaya,wakurugenzi na watendaji wengine kuhakiki yatakayofanyika katika maeneo hayo.

Sauti ya 2 Kanali Patrick Sawala mkuu wa mkoa wa Mtwara
Wananchi na wana vikundi vya ujasiria mali waliojitokeza kwenye utambulisho wa Programu ya IMASA (picha na Musa Mtepa)

Kwa upande wake katibu mtendaji wa Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Bengi Issa amesema Programu hiyo inalenga makundi ya Wanawake,vijana na makundi maalumu ambao wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kiuchumi katika kuboresha kutoka mahali alipo huku ikilenga   kusaidia wananchi.

Sauti ya Beingi Issa katibu mtendaji wa Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC)
katibu mtendaji wa Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Bengi Issa akizungumza wakati wa utambulisho wa programu ya IMASA(Picha na Musa Mtepa)