Jamii FM

DC Munkunda alipongeza baraza la madiwani Mtwara Manispaa

24 May 2024, 17:37 pm

Mkuu wa wialaya ya Mtwara Mwanahamisi Munkunda akizungumza kwenye baraza la Madiwani la Manispaa ya Mtwara Mikindani(Picha na Musa Mtepa)

niwapongeza mkurugenzi na timu yako mmefanya kazi kubwa kwenye kusimamia miradi ya maendeleo kwani kila mmoja katika kata zenu mmeweza kusimamia vizuri miradi ya maendeleo inayotekelezwa

Na Musa Mtepa

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mwanahamisi Munkunda amelipongeza na kuridhishwa na kazi inayofanywa na Baraza la madiwani la Manispaa ya Mtwara Mikindani Pamoja na wataalamu wake katika kusimamia maendeleo ya Wananchi.

Hayo ameyasema leo tarehe 24/5/2024 kwenye mkutano wa baraza la Madiwani la kupitisha taarifa mbalimbali za halmashauri robo ya tatu uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani ambapo amesema kuwa kila mmoja katika kata yake ametekeleza maagizo ya serikali ya kutumia 40% ya mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo .

Sauti ya 1Mwanahamisi Munkunda mkuu wa wilaya ya Mtwara
Waheshimiwa madiwani wa Manispaa ya Mtwara Mikindani wakifuatilia taarifa mbalimbali za utekelezaji miradi ya maendeleo ndani ya Manispaa hiyo (Picha na Musa Mtepa)

Aidha DC Munkunda ameipongeza Manispaa hiyo kwa kumaliza upungufu wa tatizo la Madawati kwa shule za Msingi ambapo amesema kuwa wakati anafika Mtwara alikuta kukiwa na upungufu wa Madawati 1,236 ambapo mpaka sasa yameshatengenezwa madawati zaidi ya 897.

Sauti ya 2 Mwanahamisi Munkunda mkuu wa wilaya ya Mtwara

Pia mkuu wa wilaya Pamoja na kuwaongezea motisha ya utendaji kazi kwa watumishi wa umma amemuomba mstahiki Meya kuwachulia hatua watumishi wazembe wasio simamia vyema katika nafasi zao.

Sauti ya 3 Mwanahamisi Munkunda mkuu wa wilaya ya Mtwara