Jamii FM
Waziri Silinde aridhishwa na ujenzi wa Bweni “Sabodo High School”
24 February 2021, 04:33 am
Naibu waziri OR-TAMISEMI anayeshughulikia elimu Mhe. David Silinde (Mb) ameipongeza timu ya menejimenti ya Halmashauri ya wilaya ya Mtwara kwa usimamizi thabiti wa ujenzi wa madarasa mawili na bweni katika Shule ya Sekondari Mustafa Sabodo ikiwa ni maboresho kuelekea kuanza kwa elimu ya kidato cha tano na sita ifikapo julai mwaka huu.
Ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani mtwara ambapo ameweza kupokea taarifa ya ujenzi wa madarasa na bweni litakalobeba wanafunzi wapatao 80 kwa wakati mmoja hivyo kusaidia kuondoa hadha kwa wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.
Pamoja na mradi huo Mhe. Waziri ametembelea na kuridhishwa na ujenzi wa Shule mpya ya msingi iliyoko Kijiji cha Hiari inayofadhiliwa na Kiwanda cha DANGOTE ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano na jamii inayozunguka Kiwanda chake kwa kutoa huduma za jamii (CSR) ambapo hadi kufikia Mwezi wa Aprili inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi.
Credit: Isaac Bilali