TADIO yaziwezesha radio za Jamii kuweka maudhui mtandaoni
22 October 2020, 09:10 am
Mtandao wa radio za jamii nchini Tanzania (TADIO) imeziwezesha radio wanachama kurusha maudhui ya matangazo ya moja kwa moja kupitia mtandao, utakaoweza kuwafikia wasikilizaji wengi ndani ya nchi na nje ya mipaka ya Tanzania.
Mafunzo ya siku mbili yakuziwezesha radio za jamii kuanza kurusha maudhui mtandaoni yametolewa na mkufunzi Markku Liukkonen kutoka Vikes Finland, yamezikutanisha radio za jamii za mikoa ya lindi na Mtwara ambazo ni Jamii Fm, Fadhira Fm na Ruangwa Fm yaliyofanyika kwenye kituo cha radio Jamii Fm Mtwara.
Katika mafunzo hayo walifundishwa namna yakuandika taarifa mbalimbali (Habari) na kuzichapisha mtandaoni pia kuweza kuunganisha matangazo (maudhui) ya moja kwa moja kupitia mtandao ambao unamilikiwa na TADIO.
Jamii Fm radio imekuwa radio ya kwanza kurusha matangazo kwa njia ya mtandao ambao umepokewa kwa furaha kwa wasikilizaji ambao walikuwa wanapata shida yakusikiliza matangazo kutokana na changamoto za masafa.
Washiriki wa mafunzo hayo kutoka radio Fadhira na Ruangwa wameipongeza TADIO kwa hatua hii yakuzipa nafasi kuweza kurusha maudhui mtandaoni kwani itawasaidia kuwafikia wasikilizaji wengi na kujiimarisha kibiashara.
ili kufatilia matangazo ya radio mtandaoni unatakiwa kutumia link hii radiotadio.co.tz/jamiifm