NSSF Mtwara yatoa msamaha wa tozo zitokanazo na ucheleweshaji wa michango ya wanachama
22 June 2024, 09:59 am
Katika utekelezaji wa shughuli za NSSF mfuko umekuwa ukikutana na changamoto mbalimbali na moja yake ni Pamoja na Mwajiri kutowasilisha michango kwa wakati na hili limekuwa tatizo kubwa kiasi kwamba inasababisha malalamiko kwa wananchi na wanachama na kudhani kwamba serikali haifanyi kazi yake ipasavyo na hii ni kwasababu wanapo kuja kwenye mfuko hawakauti fedha yao imewekwa.
Na Musa Mtepa
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) imeamua kutoa msamaha wa tozo zinazotokana na ucheleweshaji wa kulipa michango ya wanachama ikiwa katika kumpunguzia mzigo mwajiri wa kulipa michango hiyo pamoja na kujenga mahusiano mazuri yaliyopo kati ya mfuko na Mwajiri.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Juni 21,2024 Meneja wa NSSF mkoa wa Mtwara Rebule Maira amesema katika kutoa msamaha huo wametoa masharti kwenye vipengere vitatu ambavyo moja wapo ni kwa waajiri ambao watalipa malimbikizo ya michango kabla ya tarehe 31 julai 2024 watasamehewa tozo ya adhabu kwa 100%.
Aidha Bw Rebule amesema kuwa kuna waajiri ambao wanamalimbikizo yanayofikia Shilingi Bilioni 3 na wengine waliofikishwa mahakamani ambao waliomba kulipa kwanza malimbikizo ya michango ya wanachama na tozo za adhabu kutoingizwa kwenye kesi zilizopo Mahakamani na kuahidi kuzilipa hapo baadae nao watasemehewa kwa 100% .
Pamoja na hayo meneja Rebule Maira ametoa wito kwa waajiri wa Mtwara kutumia fursa hiyo kulipa malimbikizo ya michango ili kuondookana na mzigo mkubwa wa tozo za adhabu ambazo zimewekwa kisheria na zinamtaka Mwajiri kulipa ila uongozi wa mfuko umeamua kuwasamehe.
Sauti ya 3 Rebule Maira meneja wa NSSFmkoa wa Mtwara