Watumishi wa umma watakiwa kufanya kazi kwa weledi
22 April 2024, 16:30 pm
Inaonesha kumekuwa na ongezeko la vitendo vya utovu wa nidha kwa watu wa umma wakiwa kazini ikiwemo Rushwa na upungufu wa maadili.
Na Mwanahamisi Chikambu
Kamishina wa utumishi umma Balozi John Haule amewataka watumishi wa umma mkoa wa Mtwara
kufanya kazi kwa waledi na kuwataka kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi
wa umma.
Balozi John Haule ameyasema hayo leo tarehe 22-04-2024 katika ufunguzi wa kikao
kazi kati ya tume na mamlaka za serikali za mitaa Kilichowakutanisha watumishi wa umma kutoka katika
taasisi mbalimbali kilichofanyika katika ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania BOT tawi la Mtwara lengo ni kuwajengea uwezo watumishi wa serikali katika kuzitafsiri, kuzielewa sheria na taratibu zinazosimamia utumishi wa umma .
Aidha Balozi John Haule amesema kuwa riporti ya robo mwaka zinazowasilishwa kutoka kwa waajiri
inaonyesha kuwa idadi ya watumishi wa umma wanaochukuliwa hatua za kinidhamu kwa kukiuka
maadili ya utumishi imeongezeka.
Pia amewaomba watumishi wa umma kujiepusha na vitendo vya utovu wa nidhamu, kama vile
uombaji wa rushwa, uzembe, na utoro kazini ili wananchi wapate huduma zinazostahili.
Mada zilizowasilishwa katika kikao kazi hicho ni majukumu ya mamlaka ya tume ya utumishi wa umma,
haki na wajibu wa mtumishi na mwajiri, maadili katika utumishi wa umma, huku kauli mbiu ikisema kuwa
uzingatiaji wa sheria,haki na wajibu kwa kila mtumishi mwajiri na mamlaka nidhamu ndio msingi wa
ufanisi wa utumishi wa umma.