Mizengo Pinda asisitiza umuhimu wa kushikamana kwa viongozi Mtwara
21 November 2024, 11:19 am
kulingana na kanuni na taratibu za uchaguzi zinazosimamiwa na ofisi ya Rais TAMISEMI. Uzinduzi huu unahusisha vyama mbalimbali vya siasa nchini, na kampeni zitadumu hadi Novemba 26, 2024, ambayo ni siku moja kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika November 27,2024 kote nchini.
Mizengo Pinda asisitiza Umuhimu wa Kushikamana Kwa Viongozi Mtwara
kulingana na kanuni na taratibu za uchaguzi zinazosimamiwa na ofisi ya Rais TAMISEMI. Uzinduzi huu unahusisha vyama mbalimbali vya siasa nchini, na kampeni zitadumu hadi Novemba 26, 2024, ambayo ni siku moja kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika November 27,2024 kote nchini.
Na Musa Mtepa
Viongozi mkoani Mtwara wametakiwa kuendelea kushikamana, kupendana, na kuheshimiana katika ufanyaji wao wa kazi ili kuleta maendeleo kwa wananchi na kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya CCM unafanikiwa.
Hayo yamesemwa Novemba 20, 2024, na mlezi wa Chama cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Mtwara, Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Pinda amesema kuwa ili mkoa uendelee kama inavyotakiwa, viongozi wanapaswa kushikana, kusaidiana, na kuheshimiana ili mambo yaende vizuri. Amesisitiza kuwa kila mmoja anapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa maslahi ya mkoa na wananchi wote.
Aidha, Pinda amewataka wanachama wa CCM mkoani Mtwara kuacha tabia ya kuendeleza makundi ndani ya chama. Amesema chama kinahitaji wanachama wanaohimiza umoja na mshikamano ili kuhakikisha maendeleo yanaendelea kwa haraka na kwa ufanisi.
Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara, Mwal. Saidi Nyengedi, amewataka wananchi kuhakikisha wanachagua chama cha Mapinduzi huku akisema kuwa CCM inaendelea kuonesha mafanikio ya maendeleo, na kwamba kutokana na mafanikio hayo, baadhi ya wanachama wa vyama pinzani wameamua kujiunga na chama hicho.
Katika uzinduzi huo, viongozi wawili wa vyama vya upinzani wametambulishwa, Shaibu Namkuva (TUPAC) na ambao wameamua kujiunga na CCM, jambo lililoonyesha kupanuka kwa ushawishi wa chama hicho mkoani Mtwara.