Elimu ya awali, darasa la kwanza kwa wenye mahitaji maalum-Makala
21 June 2024, 10:20 am
Gregory Millanzi na Mwanahamisi Chikambu
Miaka ya nyuma baadhi ya wazazi, walezi na wananchi walikuwa wanaogopa kuwapeleka watoto wenye umri wa kuanza elimu ya darasa la awali na darasa la kwanza hasa wale wenye ulemavu na mahitaji maalum, na wengine walidiriki kuwaficha ndani kabisa.
Kwa sasa baadhi ya wazazi, walezi na wananchi wamebadilika na kuhamasika kuwapeleka shule watoto wenye ulemavu na mahitaji maalum, baada ya serikali kuboresha miundombinu ya utoaji elimu kwa darasa la awali na darasa la kwanza.
Leo tunaangazia Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kijiji cha Nanguruwe, je wamehamasika kuwaandikisha watoto kwaajili ya kuanza elimu ya awali na darasa la kwanza? Huyu hapa mratibu wa elimu kata ya Nanguruwe anatueleza hali ya uandikishaji ilivyo.