Jamii FM
Jamii FM
20 May 2025, 16:30 pm

Na Mwanaidi Kopakopa, Mwanahamisi Chikambu
Wanawake walioko katika nafasi za uongozi wamesema kuwa nafasi wanazopewa kama madiwani au wabunge zinawajengea uwezo na kujiamini kugombea nafasi nyingine za juu za uongozi wa kisiasa.
Katika makala haya, wanawake hao wameeleza kwa kina jinsi wanavyopambana kuwania nafasi za uongozi kwa njia ya ushindani wa moja kwa moja, na kuachana na uteuzi kupitia viti maalum. Wamesema kuwa mara baada ya kuingia kwenye mchakato wa uchaguzi, woga huondoka na kuwasaidia kujikita kikamilifu katika kampeni na harakati za kisiasa.
Bonyeza hapa kusikiliza makala inayoangazia viti maalumu vinavyoweza kuwa kipimo sahihi cha wanawake kuongoza katika uongozi wa kuchaguliwa na wananchi.