Maji bonde la Ruvuma, Pwani ya Kusini ni stahimilivu kwa wananchi
19 April 2024, 21:14 pm
Bonde limefanya tathmini ya maji yaliyopo juu ya ardhi na chini ya ardhi na linavituo vya kufuatilia mienendo ya maji na tunatoa vibari kwa wahitaji wa matumizi ya maji hasa kwa wanaohitaji kuweka miundombinu.
Na Musa Mtepa
Jumla ya vyanzo vya maji 81 vimeainishwa kwa ajili ya kuhifadhi ambavyo vina miradi mikubwa ya usambazaji wa maji kwa jamii katika mkoa wa Mtwara.
Hayo yamesemwa na kaimu mkurugenzi wa bodi ya maji ya bonde la Ruvuma na pwani ya kusini Bw Jaribu Modest Liana alipokuwa akizungumza na Jamii fm Radio ambapo amaesema kuwa bonde limeainisha jumla ya vyanzo 81 vinavyo jumuisha miradi mikubwa inayotumiwa na wananchi katika mkoa Mtwara.
Aidha Bw Modest amesema kuwa rasilimali ya maji iliyopo kwenye bonde la Ruvuma na pwani ya kusini ni zaidi ya mita za ujazo milioni 14.09 ambazo ukilinganisha na idadi ya watu waliopo katika bonde kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi iliyofanyika Mwaka 2022 kwa mkoa wa Mtwara ina jumla ya watu zaidi ya milioni 4.67 hivyo mahitaji ya maji kwa watu kwa kuzingati mizania ya kimataifa ni stahimilivu.
Pia Bw Modest Liana amesema kuwa moja ya jukumu kubwa linalofanywa na ofisi ya bonde la Ruvuma na pwani ya kusini ni kuhakikisha vyanzo vyote vya maji vinatunzwa na kuhifadhiwa ili viwe endelevu kwa mahitaji ya sasa na ya baadae.
Kwa mujibu wa ofisi ya bonde la Ruvuma na pwani ya kusini inaelezwa kuwa zaidi ya lita za ujazo milioni 14.09 zipo katika bonde hilo huku ikielezwa kuwa lita za ujazo milioni 11.097 ni vyanzo vinavyopatika juu ya ardhi kama vile mito,chem chem, ziwa na mabwawa na lita za ujazo milioni 3.023 zinapatikana chini ya Ardhi .