Mila ya Jando na unyago inavyo mrudisha nyuma mtoto wa kike kupigania nafasi za uongozi na maamuzi
18 April 2024, 23:38 pm
Jamii ya mikoa ya kusini tangu enzi za mababu wamekuwa na mila ya jando na unyago kwa watoto wa kike na kiume huku dhamira kubwa ilikuwa kuwatengeneza watoto kuwa heshima na busara mbele ya wakubwa hali ambayo imekuwa tofauti kwa kizazi cha sasa.
Na Musa Mtepa
Hii ni Makala inayoelezea baadhi ya mambo yanayofanyika kwenye Jando na Unyago ambayo kwa mtazamo wa jicho la tatu yamekuwa yakimrudisha nyuma mtoto wa kike kutokuwa na ujasiri wa kusimama mbele ya watu katika kupigania nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii.
Pia kupitia Mila hii imekuwa ikimtengeneza mtoto wa kiume kuwa jasiri na maamuzi mbele ya mtoto wa kike hali inayopelekea kuendelea kumdunisha Mwanamke katika jamii kutokuwa na ujasiri wa maamuzi yake binafsi pamoja na uwezo wa kugombea nafasi ya uongozi hali inayopelekea mwanamke kuwa nyuma kiuchumi,kimaendeleo na kimaamuzi.
kupitia makala haya wamesikika makungwi,mangariba,wazazi na jamii ya wanamtwara na Lindi wakizungumzia masuala mbalimbali yanayohusiana na jando na unyago.