Jamii FM

Ulemavu na Sanaa: Kipaji ndani ya sauti

17 April 2025, 15:17 pm

John Joseph Msanii mwenye ulemavu wa kuona. Picha na Msafiri Kipila

Karibu kwenye makala maalum kupitia Jamii FM, Leo tunakuletea simulizi ya kusisimua, ya kuhamasisha, na yenye kugusa hisia, simulizi ya kijana mmoja jasiri, mwenye moyo wa chuma na sauti ya dhahabu juu ya Ulemavu na sanaa

Na Msafiri Kipila

John Josephu, mzaliwa wa Mwanza, ni kijana ambaye maisha yake hayakuwa rahisi. Alipozaliwa, alikuwa anaona kama watoto wengine wote – lakini surua ilipomvamia akiwa na umri wa miaka mitano kuelekea sita, ulimwengu wake ulitumbukia gizani. Macho yake yakapoteza nuru, lakini si ndoto zake.

Na kama vile kipaji chake kilikuwa kinasubiri kuamshwa, John alianza kuimba akiwa bado mtoto mdogo. Sauti yake ikawa faraja kwake, na baadaye kuwa zawadi kwa dunia. Alipojiunga na chuo, aliendelea kuimba kwenye kwaya, na hapo ndipo jina lake lilianza kung’ara.

Lakini swali kubwa linasalia: Anawezaje kuendelea na muziki katika hali yake? Jamii inamchukuliaje? Na ni nini kinamfanya asikate tamaa hata pale wengine wanaposhindwa kuelewa?

Kusikiliza Makala haya Bonyeza hapa