SDA yapaza sauti juu ya unyanyasaji wa kijinsia
17 February 2022, 23:46 pm
Na Amua Rushita
Shirika la maendeleo ya michezo (SDA) Mtwara kupitia mradi wa kuwawezesha wabinti kupaza sauti, wameendesha Semina ya siku mbili juu ya kuwapa elimu ya namna ya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia, semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa chuo cha Montesory leo februari 16 -17, 2022.
Akizungumza na Jamii fm, Mratibu wa mradi huo Bi. Jackline mpunjo amesema semina kama hiyo inafanyika katika kila halmashauri iliyopo mkoani mtwara ili kuwajengea uwezo mabinti, waalimu na makungwi katika kupambana na ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.
Katika kuelekea siku ya wanawake duniani, wameamua kuwapa elimu hiyo ili waweze kupunguza mimba za utotoni na kuongeza ufaulu wa masomo shuleni, Pamoja na mafunzo hayo wanatarajia kugawa taulo za kike zaidi ya 450 kwa shule hamsini (50) wanazofanya nazo kazi, na taulo hizo ni rafiki kwa mazingira ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja.
Shirika hilo la Maendeleo ya Michezo (SDA) inashirikiana na serikali bega kwa bega ili kuhakikisha wanafikia malengo kwa kushirikiana na halmashuri zote za mkoa wa mtwara pamoja na dawati la jinsia.