CBT yaondoa tozo kwa wakulima wa korosho nchini
16 September 2024, 17:26 pm
Katika kuelekea msimu wa korosho 2024/2025 bodi ya korosho CBT imeamua kuondoa tozo zilizokuwa zinatozwa kwa wakulima na kuzipeleka kwa wanunuzi lengo likiwa kumsaidia mkulima kunufaika na zao hilo.
Na Musa Mtepa
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Francis Alfred amesema katika kuelekea msimu wa Korosho 2024/2025 tozo zote alizo kuwa anakatwa mkulima zimewekwa kwa mnunuzi lengo likiwa ni kumpatia mkulima fedha zake kulingana na bei itakayotangazwa kwenye mnada husika.
Hayo ameyasema Septemba 13, 2024 katika kikao cha kujadili mfumo wa ununuzi wa korosho na utaratibu wa minada kwa msimu wa mwaka 2024-2025 kilichofanyika katika ukumbi wa bodi ya korosho mkoani Mtwara
Aidha Bw. Francis amesema kuwa wanatarajia Oktoba 11,2024 kuanza ufunguzi wa minada ya zao la korosho huku akisistiza viongozi wa vyama vikuu vya ushirika magunia yao kuweka alama ili kuwadhibiti wanaonunua korosho kinyume na utaratibu .
Kwa upande wake katibu wa umoja wa wanunuzi na wasafirishaji wa korosho Omega Mnali ameshukuru kwa uwepo wa kikao hicho kwani kupitia taasisi za serikali na vyama vya ushirika vimeahidi kutatua changamoto zilizokuwa zinajitokeza katika misimu iliyopita