Jamii FM

DC Nanyumbu aapishwa, aahidi kusimamia miradi ya maendeleo

15 June 2024, 18:02 pm

Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Christopher Magala akila kiapo mbele ya viongozi wa mkoa Mtwara tayari kuitumikia nafasi yake baada ya kuteuliwa na Mh Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania hivi karibuni(Picha na Rs Habari)

Nitahakikisha ninasimamia miradi yote ya maendeleo katika wilaya ya Nanyumbu pamoja na kuwa na ushirikiano na watendaji wengine wa wilaya ili kutimiza matakwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali yake”.

Na Gregory Millanzi.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Col. Patrick Sawala leo June 15, 2024 amemuapisha Christopher Magala kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu, ambapo uapisho Umefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Rais Samia Suluhu Hassani alimteua Christopher Magala kuwa Mkuu wa Wilaya June 06, 2024 akichukua nafasi ya Dkt Stephen Isaac Mwakajumilo.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Col. Patrick Sawala amemtaka Mkuu wa Wilaya Nanyumbu ahakikishe anasimamia miradi yote ya maendeleo ambayo inatekelezwa kwenye wilaya ya Nanyumbu na kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya miradi hiyo inatumika ipasavyo kabla ya Mwaka wa fedha wa Serikali haujakamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Mtwara Col. Patrick Sawala akizungumza baada ya uapisho wa mkuu wa wilaya ya Nanyumbu
Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Christopher Magala akisaini katika kitabu cha kiapo mbele ya mkuu wa mkoa wa Mtwara Col. Patrick Sawala tayari kuwatumikia wananchi wa wilaya ya Nanyumbu(Picha na Rs Habari)

Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Christopher Magala amehaidi kusimamia Miradi ya maendeleo, amehaidi ushirikiano kwa watendaji wote wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkoa kwa ujumla ili kuwatumikia Wananchi wa Nanyumbu na Mkoa wa Mtwara kwa ujumla.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Christopher Magala akizungumza baada ya kuapishwa