Watuhumiwa 14 wakamatwa kuhusika na mali za wizi Mtwara
15 May 2024, 21:33 pm
Napenda kuwajulisha wananchi kuwa mkoa wa Mtwara upo shwari dhidi ya uhalifu na Elimu ya kuzuia na kutanzua imeendelea kutolewa kwa wananchi kupitia wakaguzi wa kata katika maeneo mbalimbali ya mkoa.
Na Musa Mtepa
Jeshi la polisi mkoa wa Mtwara limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 14 kwa kipindi cha Mwezi wa 3/ 4,2024 kwa kuhusika na upatikanaji wa mali za wizi na mtuhumiwa mmoja kukamatwa na Migomba 76 ya Bhangi.
Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari leo tarehe 15/5/2024 Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Kamishina Msaidiz Mwandamizi wa Jeshi la Polisi(SACP) Issa Suleiman amezitaja mali hizo zilizokamatwa kupitia doria iliyofanyika katika kipindi cha Mwezi wa 3/ 4 ,2024 kuwa ni pamoja na Jokofu moja aina ya mr Uk ,pikipiki nne,Tv 13 zenye aina na ukubwa tofauti .
Aidha Kamanda Issa Suleiman amesema zimekatwa pia redio Subwoofer 13 aina mbalimbali na spika zake ikiwemo Kompyuta mpakato (Laptop) aina ya HP Pamoja na ving’amuzi 32 vya kampuni ya Azam na startimes
Hata hivyo Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara limewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kukomesha matukio ya hayo.