Umuhimu wa kutunza mazingira kwa kutumia upandaji maua-Kipindi
12 February 2024, 15:07 pm
Kipindi cha Mazingira ambacho amesikika kijana Nelson Everisty mkazi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani ambae amekuwa akizalisha maua katika Eneo hilo huku akielezea namna yanavyoweza kutunza Mazingira ya Nyumbani na mengine hutumika kama Dawa na Matunda.
Na Musa Mtepa
Bustani ya maua ni moja ya vitu ambavyo vinapendezesha mazingira pamoja na uoteshaji wa matunda.
Katika shughuli hii shughuli kubwa ni kuzalisha miti ya matunda na maua, usimamiaji wa bustani za watu kwenye nyumba zao na kuhakikisha kila mteja anapata huduma kulingana na mahitaji.
Asilimia kubwa ya maua ambayo tunazalisha yanavumilia hali zote za hali ya hewa, katika hali ya joto, jua kali, mvua na hata upepo. Wanunuzi wengi wanapenda maua kwasbabu huvutia watu wengi katika kupiga picha na wengine kupumzika katika bustani hizo.
Bonyeza hapa kusikiliza kipindi hiki ambacho kinaeleza kwa undani wa ju ya bustani ya maua