Jamii FM

Mtenga Jimbo Cup Season 2 kutimua vumbi Julai 13

11 July 2024, 17:56 pm

Baadhi ya jezi zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mh Hassani Mtenga kuelekea kuanza kwa ligi hiyo season two 2024(Picha na Musa Mtepa)

Haya ni mashindano ya mpira wa miguu yaliyoanzishwa na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini ambapo mwaka huu 2024 yanaingia awamu ya pili huku takribani timu 18 zikitaraji kushiriki ligi hiyo ambapo mechi ya ufunguzi itafanyika Jumamosi ya Julai 13, 2024 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Na Musa Mtepa

Jumla ya timu 18 kushiriki ligi ya Mtenga Jimbo Cup Season two (2) 2023/2024 katika jimbo la Mtwara Mjini Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Mratibu wa mashindano hayo Iddi Musa Alli amesema ligi hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi kuanzia siku ya Jumamosi ya July 13,2024 ambapo mechi ya  ufunguzi itakuwa kati ya kata ya Vigaeni dhidi ya Kata ya Ufukoni itakayopigwa katika uwanja wa CCM  Nangwanda Siajaoni mjini Mtwara ambapo mechi hiyo itatanguliwa na mechi ya mashabiki wa Simba na Yanga

Sauti ya Iddi Musa Mratibu wa ligi ya Mtenga Jimbo cup Season two 2023/2024
Mratibu wa Mtenga Jimbo Cup Iddi Mussa Alli wa kwanza kushoto akizungumza na viongozi wa timu shiriki katika ligi hiyo juu ya ratiba na mechi za ufunguzi wake(Picha na Musa Mtepa

Akizungumza katika zoezi la ugawaji wa jezi leo July 11, 2024 Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini  Hassani Mtenga amesema kuwa ligi hiyo ni katika kuunga mkono Juhudi za Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassani katika Michezo huku akisema kuwa katika kipindi chote cha mashindano kutakuwepo timu ya watu 14 watakao kuwa wanasaka vipaji kutoka katika mashindano hayo.

Sauti ya Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Hassani Mtenga
Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Hassani Mtenga akizungumza na viongozi wa timu shiriki wa mtenga jimbo Cup juu ya dhamira ya ligi hiyo (Picha na Musa Mtepa)

Daniel Joseph Mwenyekiti wa matawi ya Simba  na Athumani Jumbe katibu wa matawi ya Yanga Mtwara Mjini wamemshuru Mbunge Mtenga kwa kitendo cha kuanzisha ligi hiyo huku wakiwaomba mashabiki wat imu zao kujaa siku ya jumamosi ya July 13,2024 kwenye mechi ya utanguzi wa ligi hiyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa matawi ya Simba na Katibu wa Matawi ya Yanga Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Naye Zuber Zuber mdau wa mpira wa Miguu mkoani Mtwara amesema amependezwa na kitendo kinachofanywa na Mbunge wa Mtwara Mjini kwa kuanziasha ligi kama hiyo kwani kwa miaka ya hivi karibuni mjini Mtwara kumekosekana muamko wa mchezo wa Mpira wa miguu ukilinganisha na kipindi cha miaka nyuma.

Sauti ya Zuber Zuber Mdau wa mpira wa Miguu mkoani Mtwara.

Mashindano haya yatahusisha timu kutoka kila kata iliyopo ndani ya Manispaa ya Mtwara Mikindani ambapo Mshindi wa Kwanza anatarajia kupata kitita cha tsh Milioni moja(1,000,000),mshindi wa pili Laki tano (500,000) na mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi Laki tatu (300,000)