Kipindi: Wenye ulemavu wanavyoweza kuibadilisha jamii kivitendo na mtazamo
11 April 2023, 12:17 pm
Na Musa Mtepa
Mifumo ya usaidizi ni muhimu ili watu wenye ulemavu waweze kuishi maisha yenye utu, waweze kujitegemea na wawe huru zaidi, haya ni maneno yaliyosemwa Machi 13 2023 kwenye mkutano wa ‘’Mtazamo wa Kimataifa wa Habari za kiutu’’ huko Geneva, Uswisi na Mtaalamu Huru wa kutoka Umoja wa Mataifa Bw Gerard Quinn kuhusu watu wenye ulemavu.
Ambapo Katika ripoti iliyowasilishwa kwenye Baraza la Haki za Kibinadamu kwa mujibu wa azimio la 44/10 la Baraza, amesema kuwa haki za watu wenye ulemavu lazima zizingatiwe ikiwepo kupata Elimu, kuishi, Afya, Malazi, chakula, Faragha na huduma nyinginezo ambazo watu wenye utimilifu wa viungo wanapata.
Leo nikikukaribishe kwenye kipindi hiki ambapo tunaangazia ni jinsi gani Watu wenye ulemavu wakipewa mahitaji sawa na wenye viungo timilivu wanavyoweza kuibadilisha jamii kivitendo na mtazamo.
Mwandaaji na msimuliaji wa kipindi hiki ni mimi Musa Mtepa wa jamii fm Radio
Kupitia kipindi hiki tunazungumza na Getrude Jonas Bukengwa Mlemavu wa miguu anaetembea kwa msaada kiegemeo(Magongo) akituelezea safari yake ya Masomo hadi kuwa Mwalimu wa shule ya msingi jamii ilivyo mchukulia lakini pia Ndoto zake kwa siku za usoni.
Naaam tumepata kusikia,kujifunza na kuelemika kupitia Dada Getrude Jonas Mwalimu wa shule ya Msingi Shangani iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani juu ya maisha aliyopitia hadi kuwa Mwalimu na matamanio aliyokuwa nayo kwa siku za usoni huku kubwa akiwataka wadau wa Elimu kam vile taasisi Binafsi na Serikali kuhakikisha wanajenga miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu na kuendelea kutoa Elimu kwa wazazi kuona umuhimu wa kuwasomesha watoto wenye ulemavu .
Aidha Mwalimu Getrude amesema kuwa jamii imekuwa na kasumba la kuwatenga watu wenye ulemavu hususani katika mahitaji ya msingi kama vile Elimu hivyo jamii iachane na kasumba hiyo na kuwapatia elimu kwa msaada wa maisha ya baadae.
Hadi kufikia hapo sina la ziada muandaaji na msimulizi wa kipindi hiki ni mimi Musa Mtepa wa jamii fm Radio Mtwara.