RPC Mtwara: Zingatieni sheria za usalama barabarani
10 April 2024, 23:17 pm
kKuvaa kofia ngumu kwa mwendesha wa pikiki ni suala la kisheria hivyo ni wajibu kwa maafisa usafirishaji (Bodaboda) wote mkoani Mtwara na abiria wake kuzingatia sheria hiyo.
Na Musa Mtepa
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP) Issa Suleimani amewataka maafisa usafirishaji (Bodaboda) na watumiaji wa vyombo vya moto barabarani kutii sheria bila shuruti ili kupumguza ajali zisizo na ulazima.
Wito huo ameutoa leo 10/4/2024 baada ya Ibaada ya Eid el-Fitir iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba mjini Mtwara ambapo amesema kuwa kuvaa kofia ngumu kwa mwendeshaji wa Pikiki ni suala la kisheria hivyo ni wajibu kwa maafisa usafirishaji (Bodaboda) wote mkoani Mtwara yeye na abiria wake kuzingatia sheria.
Pia Kamanda wa polisi amesema kuwa hali ya ulinzi na usalama katika kipindi hiki cha sikukuu umeimarika katika sehemu zote za mkoa wa Mtwara huku akiwataka Wananchi wanapotoka Kwenda matembezi wasitoke watu wote na nyumba kuiacha bila uwepo wa mtu wa kuilinda.