Waislam watakiwa kuishi maisha yanayompendeza Mwenyezi Mungu
10 April 2024, 13:52 pm
Kumewa na kutozingatia matukufu na makatazo ya Mwenyezimungu ambayo huenda ikawa sababu ya kuwepo kwa ugumu wa Maisha kutokana na Binadamu kutozingatia maagizo yake
Na Musa Mtepa
Waislam wametakiwa kuendelea kuishi Katika Maisha walivyoishi kwenye Mwezi mtukufu wa Radhamani ili kuendelea kumpendeza Mwenyezi Mungu na kuachana na vitendo vinavyo mchukiza .
Akihutubia Umma wa kiislamu uliojitokeza kwenye Ibada ya Eid fitir iliyofanyika Leo 10/4/2024 katika Viwanja vya Sabasaba Mjini Mtwara Khatwibu Ustadhi Mohamedi Salumu amesema kumewa na kutozingatia matukufu na makatazo ya Mwenyezimungu ambayo huenda ikawa sababu ya kuwepo kwa ugumu wa Maisha kutokana na Binadamu kutozingatia maagizo yake.
Aidha Khatwibu Mohamedi amesema ili kuondokana na Ugumu wa Maisha jamii haina budi kumrejea Mwenyez Mungu katika kutenda mema na kuachana na maovu.
Kwa upande Abdala Juma Muumini aliyejitokeza katika Ibada hiyo amewaomba Waislamu kuhakikisha ucha Mungu uliotafutwa kwenye Mwezi wa Ramadhani kuulinda kwa hima yote na kuishi katika Miezi iliyobakia kwa mtazamo huo ili kufikia kiwango cha Uchamungu.
Hata hivyo katibu wa shura ya Maimamu mkoa wa Mtwara Bakari Rashidi Mchira ametumia Ibada hiyo kutoa salamu kwa Serikali kuona haja ya kukaa na makampuni ya usafirishaji wa Makaay a Mawe kuzungumza na Madereva kuzingatia usalama wa watumiaji wengine wa Barabara ili kuondoa ajari zisizo na ualazima.