Mwenge wa uhuru wakabidhiwa mkoani Ruvuma
8 June 2024, 18:47 pm
Niwapongeze viongozi wote ,wa serikali na wa chama kwa kusimamia vizuri miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika mkoa wa Mtwara ,ni mpongeze mkuu wa wilaya ya Mtwara Mwanahamisi Munkunda kwa kazi nzuri aliyoionesha wakati wa mbio za Mwenge kwani amekimbiza katika halmashauri zote za wilaya Mtwara kwa ushupavu mkubwa
Na Musa Mtepa
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala leo Juni 6,2024 amekabdhi Mwenge wa uhuru katika Kijiji cha Sauti Moja kilichopo wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma ili kuendelea na mbio zake.
Akikabidhi Mwenge huo kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Sawala amesema kuwa ukiwa katika mkoa wa Mtwara umepitia miradi 62 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi Shilingi Bilioni 30.
Aidha RC Patrick Sawala amesema kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru wananchi wamenufaika kwa kukumbushwa wa jibu wa kutunza na kuhifadhi Mazingira Pamoja na kushiriki chaguzi za serikali za mitaa.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Ahamed Abbas amesema ukiwa mkoani Ruvuma Mwenge utakimbizwa katika Halmashauri 8 na kupitia miradi 72 yenye thamani zaidi ya Shilingi Bilioni 46.
Pamoja na hayo RC Ahmed Abass amesema Mwenge ukiwa mkoani Ruvuma utakimbizwa umbali wa kilomita 1289.50 huku wakitarajia kufungua Miradi 17,42 kutembelewa na kukaguliwa na 13 kuwekewa mawe ya Msingi.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava ameonesha kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo aliyotembelea katika mkoa wa Mtwara Pamoja na kuwataka kusimamia miradi yote ambayo bado haijakamilika.