Jamii FM

Kijana aliyezikwa aonekana Kijiji jirani siku moja baada ya mazishi ,Mtwara

6 December 2024, 13:17 pm

Mwonekwno wa Kaburi la kijana aliyedhaniwa kuwa Musa Ali Nasoro aliyezikwa Disemba 1,2024 katika kijiji cha Mgao Mtwara vijijini(Picha na Musa Mtepa)

Hili ni tukio la kushangaza lililotokea katika kijiji cha Mgao halmashauri ya Mtwara vijijini Mkoani Mtwara ambapo mtu aliyedhaniwa kufariki kuonekana akiwa hai siku moja baada ya Mazishi

Na Musa Mtepa

Katika hali isiyo ya kawaida, wananchi wa Kijiji cha Mgao, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Mkoani Mtwara, wamejikuta katika sintofahamu baada ya kijana mmoja anaye julikana kwa jina la Musa Ali Nasoro (40+) kudhaniwa kufariki dunia na kuonekana katika jirani cha Mbuo siku moja baada ya mazishi yake.

Akizungumzia tukio hilo, Hadija Nasoro, ndugu wa Musa Ali, amesema tukio hilo limetokea Jumamosi, Novemba 30, 2024, baada ya kupigiwa simu na watu kuwa kuna mtu amekutwa amefariki katika mlima wa Haiari-Mbuo, aliyedhaniwa kufanana na Musa, ndipo Walipoenda kumuona, kuijiridhisha kuwa ni kweli ndugu yao, na hivyo wakachukua maamuzi ya kumpeleka nyumbani na kuandaa mazishi siku ya Jumapili, Disemba 1, 2024.

Sauti ya Hadija Nasoro, ndugu wa Musa Ali Nasoro

Naye Fatuma Hamisi Sampuli, jirani wa familia ya Nasoro, pamoja na Marim Namkwanga, wamesema Musa aliondoka siku ya Ijumaa kwa ajili ya matembezi yake ya kawaida ila Walishangaa baada ya kupokea taarifa ya kifo chake, na ndipo ndugu walipoanza kufuatilia na kuandaa taratibu za mazishi.

Sauti ya Fatuma Hamisi Sampuli na Mariam Namkwanga jirani wa familia ya Musa
Nyumba anayoishi Musa Ali Nasoro kijana aliyedhaniwa kuwa amefariki (Picha na Musa Mtepa)

Mzee Abilah Tangulisa, aliyepokea maiti na kuingiza ndani baada ya kuwasili kijijini hapo, amesema ndugu walijiridhisha kuwa aliyekuwa amefariki na kuzikwa alikuwa ni Musa.

Sauti ya Mzee Abilah Tangulisa, shuhuda aliyepokea maiti
Mzee Abilah Tangulisa akielezea tukio la kuzikwa kijana aliyedhaniwa kuwa Musa Ali Kijiji Cha Mgao(Picha na Musa Mtepa)

Mzee Abilah ameongeza kuwa marehemu aliyezikwa, aliyedhaniwa kuwa ni Musa Ali, alikuwa nafanana kwa kila kitu, kuanzia mavazi, makovu, hadi mwonekano wake. Hata hivyo, kulikuwa na sintofahamu wakati wa vipimo vya uchimbaji wa kaburi, kutokana na kugundulika kuwa kaburi lilikuwa ndefu zaidi kuliko urefu wa Musa wanayemfahamu.

Sauti ya Mzee Abilah Tangulisa, shuhuda aliyepokea maiti

Kwa upande mwingine, Mzee Yusufu Shahame, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, ameielezea namna alivyopokea tukio hilo, huku akikiri kuwa aliyezikwa hakuwa Musa Ali kama ilivyodhaniwa. Mzee Shahame amewaomba ndugu na wananchi wa kijiji hicho kuwa watulivu katika kipindi hiki cha sintofahamu.

Sauti ya Mzee Yusufu Shahame, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao
Mzee Yusuf Shahame mwenyekiti wa kijiji cha Magao akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo(Picha na Musa Mtepa)