Picha ya pamoja ya Wanafunzi, walimu na wananchi wa kijiji cha Ngorongoro kata ya Nanguruwe Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, mkoani Mtwara wakiwa na Mwandishi wa Habari Gregory Millanzi wa Jamii FM kijijini hapo baada ya kuwatembelea.
Jamii FM

Miaka 62 hakuna mtoto aliyesoma darasa la awali

5 November 2024, 16:47 pm

Picha ya pamoja ya Wanafunzi, walimu na wananchi wa kijiji cha Ngorongoro kata ya Nanguruwe Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, mkoani Mtwara wakiwa na Mwandishi wa Habari Gregory Millanzi wa Jamii FM kijijini hapo baada ya kuwatembelea. 

Na Gregory Millanzi/ Mwanahamisi Chikambu

Miaka 62 iliyopita tangu kupata uhuru wa nchi ya Tanganyika na baadae kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,  kijiji cha  Ngorongoro kata ya Nanguruwe Halamashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani hapa, hakijawahi kuwa na wanafunzi waliosoma elimu ya awali kutoka kijijini hapo kutokana na umbali wa Shule ya awali na msingi ambayo ipo Kilomita 5 toka kijijini hapo hadi makao makuu ya kata ya Nanguruwe.

Wanafunzi wa Darasa la awali wa kijiji cha Ngorongoro wakiwa darasani na mwalimu wao wakiendelea na masomo. (Picha na Gregory Millanzi)

Baada ya hali hiyo kuwa kikwazo kwa watoto wao kupata elimu ya darasa kwa miaka mingi, kupitia  uongozi wa Mwenyekiti wa kijiji hicho Said Athumani Ngulyungu kwakushirikiana na wanakijiji waliamua kuanza mchakato wa kuanzisha shule shikizi hasa kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu wa kilomita 5 kufuata shule.

Kusikiliza Makala haya Bonyeza Hapa

Je Ungependa kufahamu Kuhusu Jamii FM? bonyeza hapa