Fahamu manufaa ya uwepo wa shughuli za Gesi Kijiji cha madimba katika Miradi ya Maendeleo – Makala
5 February 2024, 14:08 pm
Kwa mujibu wa SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema kiwango cha uchakataji wa gesi asilia kwa miaka nane katika kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba kimeongezeka kutoka futi za ujazo milioni 20 mwaka 2015 hadi kufikia futi za ujazo milioni 110 mwaka 2023
Na Musa Mtepa
Mkoa wa Mtwara ni mkoa uliobarikiwa kuwa na Rasilimali mbalimbali zinazojitambulisha kitaifa na kimataifa.
Rasilimali hizo ni pamoja na Kilimo cha zao la Korosho na uwepo wa Gesi Asilia Mkoa umekuwa ukitambulishwa kitaifa na kimataifa .
Gesi Asilia ambayo imekuwa utambulisho mkubwa kwa Mikoa ya kusini Lindi na Mtwara ambapo kwa mkoa wa Lindi 1974 iligunduliwa Songosongo Wilayani Kilwa na Mtwara ni 1982 katika eneo la MnaziBay kata ya Msimbati Halmashauri ya Mtwara Vijijini Mkoani Mtwara ambapo shughuli Rasmi za uchimbaji na uchakataji ulianza mwaka 2014 katika kijiji cha Madimba kilomita chache kutoka chanzo cha Nishati hiyo
Nikukuaribishe katika kipindi hiki cha Gesi na Mazingira ambapo hii leo tunaangazia uwepo wa shughuli za gesi asilia unavyowanufaisha wananchi wa madimba kupitia miradi ya maendeleo.
Mwandaaji na Msimuliaji wa kipindi hiki ni mimi MUSA MTEPA Wa Jamii fm Radio.