Jamii FM
Jamii FM
4 December 2025, 17:41 pm

Ikiwa leo ni Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani, siku hii imeambatana na mabadiliko ya tabianchi na uwepo wa mabadiliko hayo kuna athari kwa watu wenye ulemavu.
Na Grace Hamisi
Shirika lisilo la kiserikali Sports Development Aids (SDA) kupitia mradi wake wa mazingira leo tarehe 03/12/2025, wameadhimisha siku ya watu wenye ulemavu duniani kwa kushirikiana na watu wenye ulemavu kufanya usafi eneo la fukwe ya bahari na kutoa elimu namna ya kutunza takataka mkoani Mtwara.
Akizungumza mkurugenzi wa shirika hilo Tea Swai, ameelezea namna walivyoshirikiana na watu wenye ulemavu kufanya usafi huo na kutoa elimu jinsi ya kutunza mazingira pamoja namna ya kupunguza ukatili kwa watu wenye ulemavu.
Nae Afisa afya Mazingira Salome Mayala, amepongeza kwa kile ambacho kimefanyika kwani kinahamasisha watu kuweza kutunza mazingira na kujikinga na madhara yanayopatikana kwa kuchafua mazingira.
Kwa upande wake mtaalamu wa masuala ya walemavu na saikolojia, mwalimu Chris Mkwela amesema ikiwa leo ni siku ya watu wenye ulemavu imeambatana na mabadiriko ya tabia ya nchi na uwepo wa mabadiliko hayo kuna athari kwa watu wenye ulemavu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la umoja wa mataifa ambalo linahusika kupunguza hatari na majanga.
Hata hivyo Amani Danfod Kazumari ambae ni mtu mwenye ulemavu ameshukuru shirika la SDA kwa kuwakutanisha pamoja na kufanya usafiri eneo la fukwe ya bahari ambapo alikuwa mazingira sio mazuri.
Fatuma Mpondomoka mkazi wa likombe ameomba taasisi nyingine pia kuwaweka karibu watu wenye ulemavu katika shughuli mbalimbali ikiwemo siku hizi muhimu na kuwapa taarifa mapema ili wa wao waweze kujiandaa na kuonyesha vile ambavyo wanavifanya kwani wanaweza.