Nipo tayari kukatwa mguu
4 February 2023, 14:29 pm
“Wahisani na wadau wameombwa msaada wa matibu ya mguu kwa Ndg. Marias Thomas Ngole mkazi wa kitongoji cha Mijolo kijiji cha Ziwani Mkoani Mtwara baada ya kuapata ajali ya kugongwa na pikipiki miaka mitatu iliyopita.”
Na Musa Mtepa
Akizungumza na Jamii fm Radio jana Februari 3, 2023 Ndg. Marias amesema kuwa anachoomba ni msaada wa fedha au muhisani wa kwenda kumsaidia kumpeleka hospitali kutoa chuma au ikiwezekana hata kukata mguu wenyewe huku akielezea kuwa maumivu anayopitia ni makali kwani hata mfupa uliovunjika na kuungwa umeshatolewa kwa njia ya kienyeji kutokana na mguu kuoza.
“hata kutembea siwezi hali inayo nipelekea haja ndogo na kubwa kuitolea hapa hapa nilipokaa huku usingizi wangu kuupata ukiwa ni ndoto tangu miaka mitatu iliyopita” Amesema Marias.
“Hata kutembea siwezi hali inayo nipelekea haja ndogo na kubwa kuitolea hapa hapa nilipokaa huku usingizi wangu kuupata ukiwa ni ndoto tangu miaka mitatu iliyopita”
Ndg. Juma Musa Chinduli mwenyekiti wa kitongoji cha Mijolo amaethibitisha kuwepo kwa mgonjwa huyo Katika eneo lake na amewaomba watanzania kumsaidia kijana huyo anaye pitia mazingira magumu kwani wao kama viongozi wamepamabana kuhakikisha wanapata fedha za kumsaidia Bw Marias na imeshindikana kutokana na hali ya kiuchumi ya wananchi wa maeneo hayo.
Ndg. Marias Thomasi Ngole alipata ajali ya pikipiki Mwaka 2019 na kupata matibabu ya kuwekwa chuma cha kuunga mfupa wa mguu uliovunjika katika hospitali ya Nyangao Mkoani Lindi ambapo alipewa muda wa kurejea hospitalini hapo na alifanya hivyo ila kutokana na hali ya kiuchumi ya Bw Marias alishindwa kuipata fedha shilingi 200,000/= za kufanikisha kutoa chuma hicho.