Jamii FM

Utekelezaji wa ahadi za kampeni uchaguzi wa serikali za mitaa 2024

1 April 2025, 11:58 am

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyengedi Bi Lukia Mnyachi akiwa na Mratibu wa kituo cha maarifa na taarifa (KC) Coletha Chiponde wakielezea utekelezaji wa ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa 2024

Kipindi hiki kinaangazia hali ya utekelezaji wa ahadi zilizotolewa wakati wa Kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa kupitia kwa Bi Lukia Mnyachi Mwenyekiti wa kijiji cha Nyengedi ambae ni mwanamke pekee aliyefanikiwa kupata kuwa mwenyekiti wa kijiji kwa kata ya Mkunwa na ni wa pili kwa halmashauri ya Mtwara Vijijini.

Na Musa Mtepa na Mwanahamisi Chikambu

Hiki ni kipindi cha Wanawake kinachoelezea utekelezaji wa ahadi za kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa kupitia aliyekuwa mgombea ambae sasa ndiye Mwenyekiti wa kijiji cha Nyengedi kilichopo kata ya Mkunwa Halmashauri ya Mtwara vijijini Mkoani Mtwara ambapo moja ya ahadi alizozitoa wakati wa kampeni ni urejeshaji wa huduma za maji,kuundwa kwa Baraza la Wazee,ujenzi wa ofisi ya kijiji,upatikanaji wa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kijiji, Kipindi hiki kimefanywa Mubashara na Musa Mtepa na Mwanahamisi Chikambu kupitia kipindi cha Dira ya Asubuhi kinacho ruka kila siku kuanzia saa 12 : 00 hadi saa 10:00 Asubuhi.

Kipindi-Cha wanawake kinachoelezea utekelezaji wa ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa zilizofanyika 2024