Katavi:Akutwa amejinyonga chumbani kwake
22 December 2024, 10:01 pm
“Wa kwanza kubaini tukio hilo ni mke wa marehemu ambapo alikuta mlango ukiwa wazi na marehemu ananing’inia juu “
Na Samwel Mbugi -Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Boniphas Juma Katagwa mwenye umri wa miaka 34 amekutwa amejinyoga ndani ya chumba alichokuwa anaishi na mke wake mtaa wa Kigoma kata ya makanyagio manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.
Akizungumzia tukio hilo Juma katagwa baba mzazi wa marehemu amesema alisikia kelele za mayowe kutoka kwa mke wa marehemu akieleza kuwa mume wake amejinyonga chumbani baada ya kutoka kanisani majira ya saa tatu asubuhi.
Sauti ya Juma katagwa baba mzazi wa marehemu
Kwa upande wake mke wa marehemu Advera Joseph amesema aliagana na mume wake huyo kuwa anaelekea kanisani ila alipo rudi kutoka kanisani akakuta mlango uko wazi na alipoingia chumbani alikuta mume wake ananin’ginia juu ya kamba chumbani wanakolala.
Sauti ya mke wa marehemu Advera Joseph
Mama mzazi wa marehemu Maria Mashaka amesema mwanae hakuwa na changamoto yoyote na kabla ya tukio hilo kutokea alimsaidia kazi za nyumbani kwa kumtafutia kuni.
Sauti ya Mama mzazi wa marehemu Maria Mashaka
Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa wa kigoma kata ya makanyagio Athumani Lubwe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema ni tukio la pili kutokea katika mtaa wake huku akitoa wito kwa wazazi kukaa karibu na watoto wao.
Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa kigoma kata ya makanyagio Athumani Lubwe
Kamanda wa polisi mkoa wa katavi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema uchunguzi unafanyika ukikamilika atatolea ufafanuzi.