Mpanda FM

Katavi: BAVICHA waendelea na hamasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa

20 November 2024, 5:22 pm

Viongozi baraza la vijana Chadema [BAVICHA] mkoa wa Katavi.picha na Betord Chove

wamejipanga kufanya kampeni za kistaarabu na kuhakikisha wanatoa hamasa kwa vijana  Kushiriki kupiga kura huku akiomba mamlaka kutenda haki na kutofanya upendeleo kwa vyama vingine.

Na Betord Chove -Katavi

Baraza la vijana Chadema [BAVICHA] mkoa wa Katavi limeahidi  kuendelea kutoa hamasa kwa vijana kujitokeza kushiriki kupiga kura.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa baraza la vijana la chama cha demokrasia na maendeleo mkoa wa Katavi [BAVICHA] Elizabeth Pius Kasela amesema kuwa wamejipanga kufanya kampeni za kistaarabu na kuhakikisha wanatoa hamasa kwa vijana  Kushiriki kupiga kura huku akiomba mamlaka kutenda haki na kutofanya upendeleo kwa vyama vingine.

Sauti ya mwenyekiti wa baraza la vijana la chama cha demokrasia na maendeleo mkoa wa Katavi [BAVICHA] Elizabeth Pius Kasela

Aidha Kasela amegawa vipaza sauti kwa wagombea na viongozi wa baraza hilo wa nafasi mbali mbali wa chama hicho ambavyo vitawasaidia kipindi hiki cha Kampeni.

Sauti ya mwenyekiti wa baraza la vijana la chama cha demokrasia na maendeleo mkoa wa Katavi [BAVICHA] Elizabeth Pius Kasela

Kwa upande wao baadhi ya wagombea wa nafasi mbali mbali kupitia chama hicho wameshukuru kupatiwa vifaa hivyo na kuahidi kutekeleza maelekezo waliopatiwa na kiongozi wao.

Sauti za wagombea wa nafasi mbali mbali kupitia chama hicho

Kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji zimeanza tarehe 20 hadi tarehe 26 ya mwezi huu nchi nzima na uchaguzi huo ukitarajiwa kufanyika tarehe 27 ya mwezi huu.