Wafugaji wa mbwa Katavi watakiwa kuwachanja kuepukana na kichaa
29 September 2024, 8:18 am
Zaidi ya chanjo 300 zimetolewa kwa ajili ya kuendeleza kuchanja mbwa katika manispaa ya Mpanda.
Na Ben Gadau -Katavi
Katika maadhimisho ya siku ya kichaa cha mbwa duniani Septemba 28, Kampuni ya Matamba veterinary clinic imepokea chanjo zaidi ya mia 300 kwa ajili ya kuendeleza zoezi hilo la kuchanja mbwa katika maeneo mbalimbali manispaa ya Mpanda.
Akizungumza katika maadhimisho ya kilele cha siku ya kichaa cha mbwa duniani Afisa Mifugo na Uvuvi Manispaa ya Mpanda Tulinao Nswila amewaasa wananchi kujitokeza kuchanja mbwa hao ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa
Sauti ya Afisa Mifugo na Uvuvi Manispaa ya Mpanda Tulinao Nswila
Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika madhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ametoa pongezi kwa kampuni ya Matamba Veterinary clinic huku akiwataka wananchi kuona umuhimu wa kuchanja mbwa ili kupunguza madhara ya tatizo la kichaa cha mbwa.
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph
Kila ifikapo September 28 kila mwaka hufanyika maadhimisho ya kichaa cha mbwa dunia ambapo kwa mwaka huu ,maadhimisho hayo yamekuja na kauli mbiu isemayo “ondoa vizingiti vinvyokwamisha mapambano dhidi ya kichaa cha mbwa”