Mwanaume akutwa amenyongwa na mwili wake kutupwa Katavi
4 April 2024, 4:28 pm
Picha na Mtandao
“Baada ya polisi kuuchukua Mwili wa Marehemu kikosi cha ulinzi na usalama kilirudi tena kufanya Misako ya Watu wanaokunywa Pombe Saa za Kazi“
Na Samwel Mbugi-Katavi
Mtu mmoja anaekadiriwa kuwa na Umri kati ya Miaka 40-45 amekutwa amenyongwa na Mwili wake kutupwa maeneo ya Relini Mtaa wa Tambukareli Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo Selestino Shauritanga wakati akizungumza na Mpanda Radio Fm na amesema kuwa amefika eneo la tukio na kufanikiwa kuutambua Mwili wa Marehemu huyo.
Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Tambukareli Selestino Shauritanga akielezea tukio hilo
Pia shauritanga amesema kuwa baada ya Polisi kuuchukua Mwili wa Marehemu kikosi cha Ulinzi na Usalama kilirudi tena kufanya Misako ya Watu wanaokunywa Pombe Saa za kazi.
Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Tambukareli Selestino Shauritanga akielezea tukio hilo
Hata hivyo Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wamefanya msako kutokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia wema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani amethibitisha kutokea kwa tukio .Picha na Gladness Richard
Sauti Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani akithibitisha kutokea kwa tukio