Katavi, Wafanyabiashara 24 Mbaroni Kupandisha bei ya Sukari
19 March 2024, 3:19 pm
Picha na Mtandao
“Ni wajibu wa kila mfanyabiashara kuzingatia bei elekezi inayotolewa na Serikali ili kupunguza usumbufu kwa mlaji“
Na Betord Benjamin-Katavi
Jumla ya Wafanyabiashara 24 Katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamekamatwa kutokana na kuuza sukari kinyume na bei elekezi iliyotolewa na Serikali.
Akijibu swali la baadhi ya Wafanyabiashara waliohoji juu ya hali ya mwenendo wa bei elekezi ya Sukari Afisa biashara Manispaa ya Mpanda Paul Kahoya amesema ni wajibu wa kila mfanyabiashara kuzingatia bei elekezi inayotolewa na Serikali ili kupunguza usumbufu kwa mlaji
Sauti ya Afisa biashara Manispaa ya Mpanda Paul Kahoya.
Akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewataka wafanyabiashara Mkoani hapa kufanya shughuli hiyo kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa na serikali ikiwa ni pamoja na kulipa kodi.
Sauti ya Onesmo Buswelu kaimu mkuu wa mkoa wa Katavi.
Kulingana na bei elekezi ya serikali kilo ya Sukari Mkoani hapa inatakiwa kuuzwa kwa Tshs 3,200 ambapo mfuko wa sukari wa kilo 50 unatakiwa kuuzwa kwa Tshs 145,000