Wakuu wa Wilaya watakiwa kuhakiki ubora wa Miradi ya Mwenge
18 February 2023, 17:41 pm
Na Musa Mtepa
Wakuu wa wilaya na wataalamu ngazi zote wametakiwa kukagua nyaraka mbalimbali zinazotakiwa kuwepo kwenye miradi itakayopitiwa wakati wa mbio za mwenge mkoani mtwara kutekelezwa kwa ubora ili kuepuka ubadhirifu unaoweza kujitokeza.
“Navielekeza vyombo vinavyotakiwa kuchukua hatua watakapo baini i kuwepo kwa miradi iliyochini ya kiwango wasisite kuchukua hatua.”
Akizungumza baada ya matembezi ya hisani yenye lengo la kuhamasisha kuelekea uzinduzi wa Mbio za mwenge kitaifa mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abasi amesema kuwa miradi inayotekelezwa itekelezwe kwa ubora na thamani ya fedha ionekane kusiwepo na ubadhirifu wowote huku kamati zinazo takiwa kushiriki miradi hiyo ziwepo na kuhusihwa katika utekelezwaji wake.
Navielekeza vyombo vinavyotakiwa kuchukua hatua watakapo baini i kuwepo kwa miradi iliyochini ya kiwango wasisite kuchukua hatua.
Nae Mbunge wa Jimbo la Mtwara mjini Mh Hassani Mtenga ameowaomba wananchi wa Mtwara kuchangamkia fursa ya uzinduzi wa mwenge wakiwepo wafanya biashara wa nyumba za kulala Wageni, Mama Ntilie , Wasafirishaji abiria wakemo Bodaboda kujiandaa na kuitumia nafsai hiyo kujipatia kipato.
Uzinduzi wa mbio za mwenge kitaifa unatarajia kufanyika Aprili 2, 2023 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara ambapo kuelekea uzinduzi huo mkoa utakuwa na matukio mbalimbali pamoja na Wiki ya Vijana, Makongamano ya Wanawake na wiki ya Biashara.