Jamii FM

Magengeni Mtwara watakiwa kujitokeza uchaguzi serikali za mitaa

8 October 2024, 14:34 pm

Mwenyekiti wa mtaa wa Magengeni Amina Musa akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa mtaa huo(Picha na Muanya Mkoloma)

Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024 viongozi wa mitaa,vijiji na wajumbe wanatakiwa kujiuzuru ifikapo October 25,2024 .

Na Musa Mtepa

Mwenyekiti wa Mtaa wa Magengeni, Manispaa ya Mtwara Mikindani, Amina Ahmadi Musa, jana October 7,2024 amewataka wananchi wa mtaa huo kujitokeza kwa wingi katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Amina Musa amesisitiza umuhimu wa wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, huku akitumia mkutano huo kuwaaga wananchi kama sehemu ya utaratibu wa kisheria unaowataka wenyeviti wa mitaa kuacha madaraka ifikapo tarehe 25 Oktoba 2025.

Sauti ya Amina Musa Mwenyekiti wa mtaa wa Magengeni Manispaa ya Mtwara Mikindani

Naye Diwani wa Kata ya Magengeni, Ali Abdala Ali, amesema ajenda ya mkutano huo ilikuwa ni uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kujadili utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2019/2024 kwa ajili ya wenyeviti wanaotoka madarakani.

Sauti ya Ali Abdalah  Ali diwani wa kata ya Magengeni Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Diwani wa kata ya Magengeni Ali Abdala akiwa na Mwenyekiti wa mtaa huo Amina Musa kwenye mkutano uliofanyika mtaa hapo (Picha na Muwanya Mkoloma)

Fatuma Abdala, mkazi wa mtaa huo, ametoa wito kwa wakazi wa mtaa kujitokeza kujiandikisha na kushiriki katika kampeni ili waweze kusikiliza sera za wagombea na kuchagua kiongozi bora siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Sauti ya Fatuma Abdala mkazi wa mtaa wa magengeni Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Magengeni waliojitokeza kwenye mkutano