Jamii FM

Maafisa uandikishaji Mtwara DC waaswa kufuata taratibu za uchaguzi

8 October 2024, 11:57 am

Maafisa uandikishaji kutoka halmashauri ya Mtwara Vijijini wakiwa katika zoezi la kuapa tayari kwa ajili ya zoezi la uandikishaji wapiga kura katika daftari la wapiga kura (Picha na Musa Mtepa)

Ni zaidi ya maafisa 400 wa uandikishaji wa daftari la wapiga kura wameapa na kupata seimina ya jinsi ya kuanya uandikishaji katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika halmashauri ya Mtwara vijijini

Na Musa Mtepa

Mratibu wa Usimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoa wa Mtwara, Edith Shayo, amewataka maafisa uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura kufuata taratibu na sifa zinazotakiwa ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.

Akizungumza katika semina ya maafisa uandikishaji iliyofanyika Oktoba 7, 2024, katika shule ya sekondari Mustafa Sabodo, Shayo amesisitiza umuhimu wa kuelewa majukumu yao na maana halisi ya Daftari la Wapiga Kura.

Sauti ya Edith Shayo Mratibu wa uchaguzi wa serikali za mitaa mkoa wa Mtwara

Aidha Edith Shayo amesema, hana haja ya kuona zoezi likiharibiwa na ni vema kuelewe vizuri majukumu  na taratibu zinazohitajika, na kuongeza kwamba ni muhimu kwa maafisa hao kuzingatia maadili, kufuata kanuni, na kuwakaribisha vizuri wapiga kura wanaojiandikisha.

Sauti ya Edith Shayo Mratibu wa uchaguzi wa serikali za mitaa mkoa wa Mtwara
Stella Shindika hakimu mkazi akitoa maelekezo kwa maafisa uandikishaji kabla ya kula kiapo(Picha na Musa Mtepa)

Kwa upande wake, mjumbe wa kamati ya uchaguzi wa serikali za mitaa ngazi ya mkoa, Masumbuko Mtesigwa, amesisitiza kuwa uchaguzi wa mwaka huu umekuwa tofauti ukilinganisha na miaka ya nyuma kwani kila tukio  limepangwa   hivyo hakuna cha kujiongeza katika kufanikisha changamoto zaidi ya kufuata miongozo inavyoeleza.

Sauti ya Masumbuko Mtesigwa mjumbe wa kamati ya uchaguzi wa serikali za mitaa mkoa wa Mtwara.

Msimamizi mkuu wa uchaguzi halmashauri ya Mtwara Vijijini, Abeid Kafunda, amewataka maafisa hao kuheshimu sheria na kanuni zote za uchaguzi, ikiwa ni pamoja na miongozo yake.

Sauti ya Abeid Abeid Kafunda msimamizi mkuu wa uchaguzi wa serikali za mitaa halmashauri ya Mtwara vijijin.

Semina hiyo iliambatana na kiapo kutoka kwa hakimu mkazi Stella Shindika, ikihimiza umuhimu wa kufuata sheria na maelekezo katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.