Jamii FM

Dkt. Serera aitaka CBT kuimarisha ubora wa korosho kwa soko la kimataifa

15 September 2024, 11:58 am

Dkt Suleiman Serera naibu katibu mkuu wizara ya kilimo anayeshughulikia ushirika na umwagiliaji akizungumza na wajumbe walio hudhuria kikao kazi cha kujadili mfumo wa ununuzi wa korosho na utaratibu wa minada kwa msimu wa mwaka 2024-2025 (Picha na Musa Mtepa)

Soko bora la korosho huchangiwa na ubora wenyewe wa korosho hivyo wadau hawana budi kuhakikisha korosho zinazo kusanywa,kuhifadhiwa na kusafirishwa nje ya nchi zinakuwa bora kimataifa.

Na Musa Mtepa

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayeshughulikia Ushirika na Umwagiliaji, Dkt. Suleiman Serera, ameitaka Bodi ya Korosho Tanzania na bodi ya usimamizi wa stakabadhi za ghahala kushirikiana kuhakikisha korosho zinazo kusanywa, kuhifadhiwa  na kusafirishwa nje ya nchi inakuwa na ubora unaokubalika kimataifa.

Dkt. Serera amesema hayo September 13, 2024 katika kikao cha kujadili mfumo wa ununuzi wa korosho na utaratibu wa minada kwa msimu wa mwaka 2024-2025 kilichofanyika katika ukumbi wa bodi ya korosho mkoani Mtwara.

Amesema kuwa soko zuri la bei ya korosho huchangiwa na ubora wa korosho hivyo bodi ya korosho Tanzania na bodi ya usimamizi wa stakabadhi za ghalani kushirikiana katika kuhakikisha korosho zote zinazosafirishwa nje ya nchi zinakuwa na ubora unaokubalika.

Sauti ya 1 Dkt Suleiman Serera Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo  Ushirika na Umwagiliaji
Baadhi ya viongozi wa vyama vikuu vya ushirika wakiwa katika kikao kazi hicho (Picha na Musa Mtepa)

Aidha Dkt. Serera ameiomba Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA kuhakikisha inafanya kazi iliyotukuka kwa kushirikiana na mamala zingine katika kuhakikisha wakala wa usafirishaji wanaleta meli kwa wakati na zenye makasha ya kutosha ili kuondoa sintofahamu iliyojitokeza msimu uliopita.

Sauti ya 2 Dkt Suleiman Serera Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Ushirika na umwagiliaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Francis Alfred amesema katika kuelekea msimu wa korosho 2024/2025  tozo zote alizokuwa anakatwa mkulima zimewekwa kwa mnunuzi  lengo likiwa ni kumpatia mkulima fedha zake kulingana na bei itakayotangazwa kwenye mnada husika ambapo mkulima atakatwa tozo moja pekee kwa ajili ya gharama za usafiri.

Sauti ya Francis Alfred Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT)

Naye mtendaji mkuu wa soko la bidhaa Tanzania (TMX) Bw Godfrey Marekano amesema katika kuelekea msimu wa korosho 2024/2025 wamejipanga katika kuhakikisha mfumo wa ununuiz unafanya vizuri kwa wadau wote wakiwa wanatimiza majukumu yao .

Sauti ya Godfrey Marekano Afisa mtenda mkuu wa TMX

Aidha kwa mujibu wa mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania mnada wa kwanza wa zao la korosho kwa msimu wa 2024/25 utarajia kuanza Oktoba 14, 2024.