Makala: uhusiano wa matumizi hasi ya misitu na mabadiliko ya tabia nchi
9 September 2024, 11:50 am
“Tangu masika yameanza hadi kipindi hiki joto halipungui, mvua na miundombinu inaharibika kwasababu hakuna miti inayozuia mmonyoko wa ardhi”
Na Musa Mtepa,
Uhifadhi wa misitu unasimamiwa kisheria ambapo inatambulika na sheria za Tanzania na pia kabla kuvuna mazao ya misitu, inashauriwa kuwasiliana na watalaamu wa TFS ili wakupoe mbinu bora za uvunaji huo
Katika makala haya umehoji juu ya uhusiano wa matumizi hasi ya misitu na njia za kukabidiriana na mabadiriko ya tabia ya nchi, tumetembelea katika Kijiji cha Namayakata shuleni na Kijiji cha Nyengedi ili kupata maoni yao.
Salumu selemani Mtunuma Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha nyengezi anasema anafahamu suala la uvunaji wa miti, na tunavuta miti ya aina nyingi hasa kwaajiri ya ujenzi na mkaa, sisi tunakata miti ya mkaa kitu ambacho hali inayobakia basi mazingira yanabadirika, na sasa hivi miti haiwi mikubwa sana.
Tangu masika yameanza hadi kipindi hiki joto halipungui, mvua na miundombinu inaharibika kwasababu hakuna miti inayozuia mmonyoko wa ardhi, sasa tunaangalia namna ya kufanya sheria ili hapa namayakata paweze kurejea kama mwanzo ambapo tulikuwa tunavuna sana sasa hivi tabia ya nchi imekuwa tofauti Azizi hasani serikali ya Kijiji cha Namayaka shuleni