Jamii FM

NEMC kanda ya kusini yawataka vijana kuchangamkia fursa za kimazingira

3 June 2024, 12:33 pm

Meneja wa baraza la taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira(NEMC) kanda ya kusini Mhandisi Boniphace Guni akizungumza wadau wa mazingira wakati wa mdahalo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha stella Maris Mtwara (Picha na Musa Mtepa)

Kongamano hili ambalo limehusisha wadau mbalimbali wanataaluma,wanafunzi ,taasisi za serikali na binafsi huku matarajio ya ujumbe kufika ukiwa mkubwa kwa wadau kwani kumekuwa uwasilishaji wa mada mbalimbali hasa kwa upande wa zao la korosho na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Na Musa Mtepa

Wananchi na wadau wa mazingira wameombwa kufanya shughuli zinazosadia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwa njia moja wapo ya kurejesha uoto wa asili na utunzaji wa Mazingira.

Wito huo umetolewa tarehe 2/6/2024 na Mhandisi Boniphace Guni meneja wa baraza la taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) kanda ya kusini  kwenye kongamano la vijana kuhusu fursa za kimazingira lilizofanyika katika chuo cha Stella Maris Mtwara ambapo amesema kuwa wadau wa mazingira hawana budi kufanya shughuli ambazo zitasaidia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia Pamoja na kuendelea kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira.

Sauti ya 1 Mhandisi Boniphace Guni Meneja wa NEMC kanda ya kusini
Meneja wa NEMC kanda ya kusini Mhandisi Boniphace Guni wa pili kutoka kushoto akiwa na wawasilisha mada katika kongamano la vijana kuhusu fursa za kimazingira(Picha na Musa Mtepa)

Aidha akijibu swali la mchangia mada aliyehitaji kufahamu ni mikakati gani NEMC imeweka katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira katika eneo la Bahari Mhandisi Guni amesema kuwa  serikali imeandaa taarifa na miongozo ya namna bora ya njia zipi zitumike katika kuhakikisha kwamba zinapunguzwa athari hizo.

Sauti ya 2 Mhandisi Boniphace Guni Meneja wa NEMC kanda ya kusini

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa bodi ya korosho Tanzania Francis Alfred amesema vijana wana fursa kubwa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kupitia zao la korosho ikiwemo kuanziasha viwanda vya ubanguaji wa korosho,uuzaji na kuwekeza katika kilimo cha korosho.

Sauti ya Francis Alfred Mkurugenzi mkuu wa bodi ya korosho Tanzania

Mkurugenzi wa Bodi ya korosho Tanzania Francis Alfred akiwasilisha mada ya fursa za mabadiliko ya tabia nchi katika zao la korosho kwenye kongamano la vijana lililofanyika tarehe 2/6/2024 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Stella Maris Mtwara (Picha na Musa Mtepa)

Hili ni kongamano lililolenga kutoa Elimu kwa wadau mbalimbali hasa kwa vijana kuona fursa gani zinazoendana katika urejeshwaji wa ubora wa Ardhi ,kukabiliana ya hali ya jangwa na ustahimilivu wa hali wa ukame .

Wadau wa mazingira waliojitokeza katika kongamano la vijana kuhusu fursa za kimazingira(Picha na Musa Mtepa)