Jamii FM

Kamati ya Bunge yaipongeza Serikali umiliki wa Gesi Asilia

25 March 2024, 14:54 pm

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya uuma Mh Deus Sangu akiwa na wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia Cha Madimba Mkoani Mtwara. (Picha na RS Mtwara)

Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma imeipongeza serikali kwa kuchukua hatua ya kuwasomesha vijana wa kitanzania nje ya nchi ambao kwasasa ndio wanao simamia mitambo ya kuchakata na kuzalisha Gesi Asilia katika kjiji cha Madimba Mkoani Mtwara.

Na Musa Mtepa

Kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma imesema kitendo cha serikali kuongeza hisa kwenye sekta ya gesi asilia kumefanya nchi kunufaika zaidi na rasilimali hiyo inayotarajiwa kukuza uchumi wa taifa.

Hayo yamebainishwa March 24,2024 na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma Deus Clement Sangu,walipotembelea viwanda vya kuchakata Gesi Asilia cha mnazi Bay na Madimba  Halmashauri ya wilaya Mtwara mkoani Mtwara.

Amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada kubwa za uwekezaji hasa uliofanyika Mwezi Februari, 2024 kwaa kuingia katika rekodi ya nchi ambapo Shirika la Maendeleo ya Petrol nchini (TPDC) imeongeza 20% za hisa  na kufanya shirika hilo kuwa  na umiliki wa 40% na 60% zinabaki za mwekezaji.

Sauti ya Deus Sangu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge uwekezaji wa mitaji ya umma.

Kwaupande wake Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Vuma Agustino, ameipongeza serikali kuchukua hatua ya kuwasomesha vijana wa kitanzania nje ya nchi ambao kwasasa ndio wanao simamia mitambo hiyo ya kuchakata na kuzalisha gesi.

Sauti ya Vuma Agustino Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC Balozi Ombeni Sefue amefurahishwa na ujio wa wakilishi hao wa Wananchi katika kuwaonesha jinsi fedha zinavyotumika na mchango unaotolewa kupitia sekta ya Gesi na kusistiza  kuwa watahakikisha rasilimali hiyo inatumika katika kubadilisha  maisha ya watu pale ambapo Gesi Asilia inapatikana na kutoa mchango mkubwa kwa uchumi wa taifa.

Sauti ya Balozi Ombeni Sefue Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC