Walemavu waomba kupewa kipaumbele cha Elimu na Ujuzi
25 November 2021, 11:26 am
uwepo wa mikataba ya ya haki za watu wemye ulemavu Tanzania inafuatwa? uwepo wa taasisi zinazosaidia watu wenye ulemavu wanafikia malengo na wahusika wanapewa stahiki klulingana na miradi husika?
Mr. Kaganzi
Na MUSSA MTEPA;
Serikali na taasisi binafsi zimetakiwa kutenda na kuwapatia mahitaji ya msingi ikiwepo Elimu na ujuzi kwa watu wenye ulemavu ili kuwezesha kujikimu katika kujipatia kipato kama wengine na kuodokana kuwa tegemezi.
Akizungumza katika ufunguzi wa Warsha ya kuwawezesha kutambua na kutofautisha baina ya watu wenye ulemavu na wenye mahitaji maalum Mr Rutachwamagyo Kaganzi
amesema kuwa kwa nchi yoyete iliyoridhia mkataba wa haki za watu wenye ulemavu kama Tanzania hainabudi kufuata matakwa ya mkataba huo kama inavyotakiwa huku akisema kwamba hawatakiwi kuangalia sehemu moja tu katika nyanja ya Elimu waangalie pia baada ya kupata Elimu anawezaje kuitumia Elimu hiyo akiwa mtaani.
Aidha Mr Kaganzi amesema kuwa taasisi zinazo saidia watu wenye ulemavu zinapoanzisha mpango kwa walemavu zihakikishe zinawajengea uwezo wahusika ili inapofikia tamati mlemavu aweze kunufaika binafsi na jamii inayomzunguka na sio kuwa mzigo tena.
Kwa upande wake Mwalimu Kusaga kutoka chuo cha ufundi stadi VETA Mtwara amesema kuwa katika kuunga mkono jitihada za serikali na taasisi binafsi wamekuwa wakipokea watu wenye ulemavu katika chuo hicho na kuwapatia Elimu ya ufundi inayowasaidia kujipatia kipato pindi wamalizapo wakiwa mtaani na kutanabaisha kuwa kumekuwa na walemavu wamekuwa wakifanya vizuri katika masomo kuwapita hata waliokamilika .
Pia Bi Kusaga amesema kuwa jamii haina budi kuwapa nafasi watu wenye ya kupata Elimu kama wengine kwani inasaidia kuondoa hali ya utegemezi katika familia.
Naye Bi Zena Shayo kutoka kituo kikubwa cha polisi mkoani Mtwara amesema kuwa wao kama jeshi la polisi wamekuwa wakisaidiana na wadau mbalimbali katika jitihada za kulinda watu wenye ulemavu kupata haki za msingi kutoka kwa wanafamilia na jamii kwa ujumla hasa inapotokea hali ya kiukatili na unyanyasaji kwa watu hao.
Bi Thea Swai ni meneja wa mradi wa empowered Girls speak out ulio chini ya taasisi Binafsi ya sports aid Development (SDA) katika Mkoa wa Mtwara amesema kuwa warsha hiyo ipo chini ya mradio wenye lengo la kuwawezesha ,kuwajengea uwezo wataalamu mbalimbali kujifunza kuhusiana na watu wenye ulemavu haki zao kwa ujumla , maana ya kuwashirikisha,kuwapa majukumu na namna ya kuwafikishia taarifa mbalimbali zihusuzo shughuli na maisha kwa ujumla.